Katika ule mpango wa marvel kutoa movie na series mbalimbali za masuper heroes sasa yaja kwa kishindo na series mpya inayotegemewa na wapenzi wengi wa filamu kuwa itaweza kufanya vizuri
baada ya ile filamu ya daredevil ya mwaka 2003 iliyoigizwa na Ben Affleck kufanya vizuri hivyo hivi sasa wameamua kuitengenezea series ambayo itaanza rasmi April 10 /2015 . Hivyo wapenzi wa filamu wakae tayari.
Baada ya mazungumzo ya muda mrefu kati ya kampuni ya SONY na MARVEL kuhusu kumtumia SPIDERMAN katika muendelezo wa filamu za AVENGERS atimaye kampuni ya SONY imekubali MARVEL kumtumia spiderman kama moja ya wahusika wakuu katika filamu za avengers katika makubaliano yao marvel haitokuwa na kibali cha kutengeneza movie binafsi ya spiderman bali itaisaidia sony kutengeneza movie mpya ya spiderman itakayokuwa na maboresho ilikuwa bora zaidi ambayo itatoka 2017.
The flash ni series iliyojipatia umaarufu mkubwa ndani ya muda mfupi ulimwenguni kote na kujizolea mashabiki wa kutosha ikiwa ndo kwanza ina episode 13 tu za season ya kwanza. Hii ni katika mpango ule wa DC comics kuwatengenezea masuper heroes mbalimbali series zao binafsi zinazojitegemea baada ya kuona hile series ya ARROW imepokelewa vizuri na wapenzi wa filamu hivyo wameendelea na mfurulizo wa kutoa series mbalimbali za masuper heroes na nyingine ambazo zipo njiani kutoka.
Wale wale wataalamu wa kuchonga mbavu za plastic, aka wachekeshaji balaa..sasa wameingia na kitu kipya kwa jina Zena & Betina, amini usiamini nikikusimulia namaliza uhindo. Jipatie nakala yako sasa